ARUBAINI YA SUNGURA
na Yussuf Hamad


Hapo zamani za kale walikuwepo wanyama mbalimbali ambao
waliishi kwa pamoja na kushirikiana kwa kila kitu. Siku mmoja Simba; mkuu wa
wanyama aliitisha mkutano wa wanyama wote. Wanyama wote wailitikia wito.Siku ya
kikao ilipofika wanyama wote walihudhuria katika mkutano huo muhimu wa wanyama.
Simba alihutubia wanyama wote na kuwataka wachimbe kisima kwa sababu kulikuwa
hakuna maji katika mito na maziwa. Wanyama wote walikubali rai hiyo ya mfalme
Simba. Siku ilipofika wanyama wote walikutana na kuanza kuchimba kisima
isipokuwa sungura tu. Sungura hakutaka kushirikiana na wanyama kuchimba
kisima.Fisi alitumwa na mfalme simba akamuulize sungura kwanini hakuja
kushiriki katika kuchimba kisima. Fisi alikwenda hadi nyumbani kwa sungura.
Huko alimkuta sungura akiwa barazani akichambuwa karanga kwa ajili ya chakula
chake cha mchana. Fisi alimsalimia sungura; ``Hujambo sungura?’’ Sungura
alinyanyua uso wake na kumtazama fisi kisha akaitikia ``Sijambo fisi. Habari za
siku nyingi?’’ Fisi nae aliitikia kwa kusema; ``Mimi sijambo pia! Ila tu
nimetumwa nije kukuuliza kwa nini hujashiriki katika ujenzi wa kisima?’’ Fisi
alimuuliza sungura.Sungura nae alicheka kidogo kisha akamwambia fisi; ``Mimi
sina haja ya maji kwani nina maji yangu matamu sana. Maji mnayochimba yana
matope na ni machafu. Mimi sipendi maji yenye matope. Nyinyi chimbeni kisima na
mimi sitokunywa kamwe maji yenu hayo machafu!’’
Fisi aliondoka nyumbani kwa sungura na kuelekea kwa mfalme
Simba. Alipofika alimweleza yote aliyoelezwa na sungura. Simba alisikitika sana
aliposikia majibu ya sungura ambayo yalijaa kebehi na dharau kwa wanyama
wengine. Lakini simba hakumchukulia sungura hatua yoyote. Baada ya siku kupita
kisima kilimalizika na wanyama walianza kutumia maji. Kisima kilitoa maji mengi
sana na wanyama wote walifurahi. Baada ya siku tatu tu tangu kisima kimalizike
na watu waanze kuchota maji wanyama waligunduwa kitu amabacho si cha kawaida
pale kisimani.
Kila wakifika kisimani asubuhi waliona maji yamechafuliwa sana
na kuingizwa takataka nyingi. Hivyo wanyama walimwambia Simba kuhusu uharibifu
huu. Simba alifika kisimani siku iliyofuata na kuona maji yamechafualiwa sana.
Simba aliamuwa kuweka ulinzi pale kisimani ili kumkamata anaeharibu maji. Hivyo
zamu ya kulinda kisima ikapangwa. Mnyama wakwanza kuanza kulinda kisima alikuwa
tembo. Tembo alilinda kisima usiku na alikuwa amejificha kichakani kumdoea
mchafuzi wa maji kisimani. Ilipofika usiku wa manane, Tembo alisikia kiumbe fulani
kinakuja. Tembo alikaa tayari kumkamata mchafuzi wa maji.Mnyama huyo alikuja
hadi kisimani na alikuwa Sungura. Sungura alichota maji, kisha akakoga na
baadae akaanza kuyachafua. Tembo alitoka kichakani na kumshika Sungura. Tembo
alimwambia Sungura;``Leo nimekushika mchafuzi wa maji. Sikuachi hapa mpaka
asubuhi nikupeleke kwa mfalme Simba ili ukapate adabu.’’ Sungura alicheka sana
na kumwambia Tembo; ``Mimi sio muharibifu wa maji.Kwanza mimi sinywi maji haya.
Maji haya si safi na wala si matamu. Mimi nina maji yangu matamu sana.’’
Sungura alitoa kichupa kidogo cha asali. Kisha akamwambia Tembo;`` Unaona haya
ndio maji
ninayokunywa mimi. Haya ni matamu sana.’’ Tembo alishangaa
sana na alimwambia Sungura tafadhali nionjeshe kidogo maji yako.’’ Sungura
alimuonjesha Tembo ile asali ambayo alidai ni maji. Tembo alionja kidogo na kwa
vile ilikuwa tamu alimwambia Sungura;’’ Tafadhali niongeze tena’’. Sungura
alimwambia Tembo; ``Hapana! Siwezi kukuonjesha mpaka nikufunge katika mti kwani
utanizidi nguvu na kuninyang’anya maji yangu matamu’’. Tembo alikubali na
Sungura alimfunga Tembo katika mti mkubwa halafu akamcharaza viboko mpaka Tembo
alikaribia kufa. Hapo sungura alimwambia Tembo nitakuachia lakini usimwambie
mtu kuhusu mimi. Tembo alikubali na Sungura aliondoka na kumwacha Tembo akiwa
amefungwa pale mtini. Asubuhi wanyama walipokuja walimkuta Tembo amefungwa
amelala akiwa taabani. Walimuuliza kulikoni lakini tembo hakusema kitu. Siku
iliofuata ilikuwa zamu ya Fisi.
Nae alipata kipigo kama Tembo, kisha akaja
punda ambae pia aliambulia kipigo. Wanyama wote waliopangwa walipigwa sana na
Sungura.Akawa amebaki kobe. Kobe alimwambia Simba mimi nitaweza kumkamata
mchafuzi wa maji. Wanyama wote walishangaa na kumwambia kuwa hataweza kwani
wameshindwa wanyama wakubwa hivyo yeye hatoweza. Kobe alisema nitaweza na
alikwenda kisimani. Alipofika alijipaka ulimbo mgongoni kwake. Sungura alipofika
hakujua kuwa alikuwepo kobe hivyo aliona kuna jiwe tu pale kisimani. Sungura
alipanda juu ya mgongo wa kobe. Mara
miguu yake iliganda.Sungura akasema; ``Umeikamata miguu yangu sio? Nina mikono
pia’’. Sungura alipeleka mikono yake. Mikono ikanasa katika ulimbo na sungura
akawa hawezi kutoka.asubuhi wanyama walipokuja walimkuta kobe akiwa ameganda
mgongoni kwa kobe hana la kufanya. Kobe alimkabidhi sungura kwa samba kwa ajili
ya kuhukumiwa. Wanyama wote walimpongeza Kobe kwa kazi yake nzuri.
Kazi nzuri kwa wanafunzi wachanga.Itaweza kukuza vipawa vyao vya uandishi
ReplyDeleteKazi nzuri sana
ReplyDeletenimefurahi sana nipikuwa naitaftaa xana🤣🤣
ReplyDeleteHongera sana umetukumbusha mbali
ReplyDelete